Audio: Wynem - Utata
Hii hapa ngoma ya Wynem iliyotengenezwa pale Jalaman Records na mtayarishaji akiwa Jalaman mwenyewe. Ingawa ilikuwa 2010 lakini bado sauti ya Wynem iliendelea kufanya poa.
Wynem aliwahi kutoa ngoma yake ya Mwanambuzi iliyowahi kutesa baadhi ya redio za Dar.
Pia Wynem amewahi kushirikiana na Linex a.k.a Sunday Mjeda katika ngoma kama vile Maumivu, Japo Kidogo na nyingine kadhaa.
Si hivyo tu, aliwahi pia kunogesha ngoma za Raph Tz ambazo ni "Kauli Safi" na "Hisia Zangu" na Suma Mnazalet katika "Tofauti na Jana" kwa viitikio vikali.
Nick Maujanja pia atamkumbuka Wynem katika video ya wimbo wake Sms
0 comments: