Baby Madaha: Asema Anawapanga Foleni Wanaume
Msanii wa muziki na filamu za Bongo, Baby Madaha ambae anadaiwa kuishi kinyumba na meneja wake Mkenya, Joe Kariuki wa Kampuni ya Candy n Candy Records, ametoa mpya baada ya kudai kuwa kutokana na kusubiri kwa muda mrefu ili apate mwanaume anayefaa kwa ajili ya kumuoa bila mafanikio, sasa ameamua kuwapanga foleni bila kujali idadi yao.
Akipiga stori na chanzo fulani cha habari, Madaha alisema amesubiri sana kuolewa lakini hajamuona mwanaume anayefaa, hivyo ameamua kuwapanga kama mafungu ya nyanya kama wao wanavyowapanga wanawake na ikitokea mmoja akamzingua anaachana naye na kumchukua mwingine.
Asema;
"Mimi sasa hivi nawapanga tu wanaume maana sioni anayenioa ndiyo maana nimechukua uamuzi huo, wanaume wamezoea kutupanga sisi wanawake sasa mimi ndio nimewageuzia kibao nao waone utamu wake na ikitokea huyu amenizingua namuacha nahamia kwa mwingine"
0 comments: