Wamama 6 Tegemeo Bongo Movie

Katika kila fani kuna watu ambao wanaonekana kuwa tegemeo au nguzo kubwa kulingana na nafasi husika. Katika tasnia ya filamu Tanzania, kuna wamama ambao ni wakongwe na mara nyingi wanapopewa nafasi hufanya kweli na kudhihirisha kwamba uigizaji uko kwenye damu..

Akina mama 6 japo umri umeenda lakini bado tasnia hiyo ya uigizaji inawahitaji na bila wao pengo kubwa litaonekana.

#1. Hidaya Njaid
Kwenye picha kushoto. Aliwahi kucheza kama mama wa Vincent Kigosi "Ray" na marehemu Steven Kanumba katika filamu ya "Off Side" amabyo alionyesha umahiri mkubwa tofauti na wasanii wanaoibukia sasa hivi.


Pamoja na hiyo, pia amecheza filamu nyingine kama vile Shakira, Mtumwa, Family Apart, Lose Control na nyingine nyingiiiiiiiiiiiiii.


#2. Fatuma Makongoro "Bi Mwenda"


Ni mama ambae huwa ananoga sana akiigiza filamu za kuhusu uchawai au zile zinazoonyesha manyanyaso. 

Bi Mwenda amewahi kucheza filamu kama vile True Love, My Princess, Ukungu, Loreen, Mtoto wa Kitaa, Jungu la Urithi na nyinginezo.









#3. Grace Mapunda "Mama Kawele"


Huyu ni mama anayecheza kwa hisia na anajulikana kwenye sanaa akiwa kwenye kundi la Splendid lililokuwa na makazi yake Ilala Bungoni ambalo pia liliwatoa kina JB, Mau na wengine wengiii lililokuwa chini ya Ticha.

Mara nyingi hucheza kama mwanamke anayenyanyasika na huwa mwepesi kutoa machozi.

Filamu alizoigiza ni kama vile Family War, My Life, Five Girls na nyingine nyingi.




#4. Suzan Lewis "Natasha"

Mama huyu ana umaarufu mkubwa ndani ya tasnia ya filamu Bongo na amecheza filamu nyingi katika nafasi ya mama. Pia amecheza filamu na mwanae halisi Yvone Cherry Ngatwika 'Monalisa' iliyokwenda kwa jina la "Chanzo ni Mama".

Pia amecheza In Between, Msukule, Cross My Sin, The Twins na nyingine nyingi.





#5. Thecla Mjata "Mama Mjata"

Huyu alianzia kwenye maigizo ambapo alikamua vilivyo katika igizo la "Usilolijua Usiku wa Giza". 

Mpaka sasa mama huyu ni tegemeo kwa filamu mbalimbali za Kibongo akicheza kama mama.

Mama Mjata anajua kucheza kwa hisia na ameigiza filamu nyingi zikiwemo "Hazina ya Marehemu", "Kolelo", "Back from America" na nyingine kibaaaaaaoooo.





#6. Herieth Chumila

Ni mama anayefanya vizuri kwenye filamu na pia kwa umahili amewahi kuchaguliwa kuwa mama mlezi wa wasanii wa Kundi la Bongo Movie Unity.

Amewahi kushiriki katika filamu kama vile Vanessa, Dillema, Witch Doctor, Shortcut, Surprise, Gentleman, Illegal Sister na nyingine nyingi.

0 comments: