Vita Baridi: Ali Kiba v. Diamond Platnumz

MCHUANO: 
Tamasha la Fiesta 2014 limepita lakini nyuma yake limeacha vita nzito iliyowahusisha mafahari wawili, Ali Kiba na Nassib Abdul "Diamond" 

Mchuano Ulivyokuwa
Kwenye show hiyo iliyofanyika wikiendi iliyopita katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es Salaam, mashabiki wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Ali Kiba (Team Kiba), walipiga kelele za 'buuu' pale alipopanda Diamond kutumbuiza ili kumharibia.




Ukweli wa Mambo
Chanzo chetu kimedai kuwa vurugu hizo hazikutokea kwa bahati mbaya bali zilipangwa na wafuasi wa Kiba ambapo inasemekana ziliandaliwa gari aina ya Toyota-Costa zipatazo 25 zilizokuwa zimejaa watu na kwenda kuwamwaga uwanjani hapo kwa shughuli mbili muhimu; kuzomea na kuhamasisha wengine wazomee pindi Diamond atakapopanda jukwaani.

Kwa namna moja ama nyingine mashabiki hao walionekana kufanikiwa kwani waliweza kuwashawishi watu wengi wazomee kiasi cha kumfanya Diamond anshtukie na kutamka hadharani: "JAMANI KUNA UHUNI UNAENDELEA HAPA"

Team Diamond Wacharuka
Madai yanasema mara baada ya Team Kiba kufanya vurugu hizo na kufanikiwa, baadhi ya mashabiki ambao waliaminika ni wa Diamond (Team Diamond) walicharuka na kusema hawakubaliani na uhuni huo ambao umefanywa hivyo na watahakikisha wanapambana kulipiza kisasi kwa namna yoyote ile.


0 comments: