Rose Ndauka: Wanaume Mnikome
Baada ya kuonja joto la kuishi mwenyewe sasa msanii wa filamu Rose Ndauka, amesema kuwa haihitaji tena kusikia suala la kuishi na mwanaume au kuolewa kwani kila kitu anakifahamu juu ya maisha yao.
Alisema, "Sasa hivi nahitaji kutulia pengine hata miaka mitano sitakuwa na mtu najua mahusiano kwani kwa upande fulani yanirudisha nyuma kimaisha. Ni kweli mapenzi yana raha lakini kwangu nahitaji kupumzika ili niweze kutafakari nini cha kufanya kwa ajili ya kukuza sanaa yangu.
Rose Ndauka alishawahi kuolewa na kumkimbia mumewe ambae alikuwa mmoja kati ya wasanii wa kundi la TNG Squad toka Tanga waliotamba na wimbo "Bongo.Com"
0 comments: