Video | Nuh Mziwanda ft. Ben Smart - Amina

Msanii wa Bongofleva na aliyewahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii na mmiliki wa mgahawa wa Shishi Food, Shilole, kijana mtanashati Nuh Mziwanda, ameendelea kufanya vizuri katika muziki wa kizazi kipya.
Nuh alikutana na Bongo Focus pande za THE RETURN LOUNGE ya Mwenge Dar es Salaam na kufunguka kwamba bado ataendelea kupambana kufanya kazi nzuri kwa mashabiki wake na kuhakikisha mtoto wake anapata malezi bora kupitia kazi yake ya sanaa.
Akiwa ameshirikiana na Ben Smart, hii hapa ni kazi yake ya video aliyoitoa hivi karibuni. Kazi imefanywa na Kwetu Studios.
Enjoy!

0 comments: