Ujio Mpya wa Raph Tz akiwa na Tundaman na Darasa; Jipange
Akiwa anatokea Dodoma na kuiwakilisha vizuri Dar, msanii, mwanamuziki wa miondoko ya kufokafoka, Raph Tz ama Raph Tanzania amepanga kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la "JIPANGE".
Ngoma hiyo imefanywa katika studio mbili tofauti, ya Kijitonyama, Dar (Kali Nation) kwa mtayarishaji Jaysson na kumaliziwa Dodoma kwa Double studio za G Sound Records zilizopo Kisasa.
Bila hata kupoteza point yoyote, Raph Tz amejijengea msingi mzuri wa kufanya na wasanii wawili wakali wanaotamba katika mziki Tanzania, nawazungumzia Tundaman "Mzee wa Msambinungwa" na Darasa "Mr Sikati Tamaa".
Pia Raph ameamua kuachia beat/mdundo wa wimbo huo kama maandalizi au kionjo cha wimbo wake huo mpya.
God bless him
0 comments: