Davido Azidisha Utata Kati ya Times Fm na Clouds Fm
Msanii kutoka Nigeria, David Adedeji Adeleke ama maarufu kama DAVIDO ameendelea kuongeza chachu ya utata uliopo kati ya Clouds Fm na Times Fm.
Hii ni baada ya Davido kupanda jukwaa la FIESTA na kutumbuiza ilhali akiwa amewekewa pingamizi la kibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) sambamba na zuio la Mahakama ya Kisutu lililowekwa na Redio Times Fm waliodai kuwa na mkataba kufanya nae show, Novemba 2014.
Times Wafunguka
Mkurugenzi wa Redio Times Fm, Rehure Nyaulawa alipotafutwa kwa simu kuhusiana na suala hilo alisema mahakama ilishaweka pingamizi, anashangaa kuona msanii huyo alipanda jukwaani lakini akasema hawezi kukaa kimya, atakwenda mbele zaidi ili haki itendeke
Clouds Fm Mitini
Clouds walipotafutwa hawakupatikana hewani lakini kimsingi na wao wana hoja zao ambazo zitabainika pindi kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.
Hata hivyo kuna madai kwamba, zuio la Davido kutopanda jukwaani Leaders Club lilipelekwa na mahakama kwa Clouds Media Group wakati Tamasha la Fiesta linaandaliwa na Kampuni ya Primetime Promotion, kwa hiyo barua hiyo ilikuwa "missing in action"
0 comments: