Miss Tanzania Ajikanyaga Suala la Passport na Leseni Yake

Mwanadada anayeshikilia taji la Redds Miss Tanzania, Sitti Mtemvu ameingia katika wakati mgumu sana na kuzidi kuendelea kujikanyaga ili kuendelea kutetea taji hilo.
Sitti ambaye inasemekana mwanzoni mwa mashindani ya kinyang'anyiro hicho alisema kuwa ana miaka 18, lakini baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii, akakanusha kuhusu miaka yake, na kusema ana miaka 23.
Katika kikao kilichofanyika tarehe 20.10.2014 baina ya kamati ya Miss Tanzania na waaandishi wa habari, Sitti ameonekana akikosa cha kuongea baada ya kubanwa sana na maswali.


Sitti Ajikanyaga
Sitti alijikanyaga pale alipoulizwa mbona cheti chake cha kizaliwa kinaenda tofauti na takwimu za passport yake pamoja na leseni ya udereva, na kubaki kutokuwa na majibu ya kuridhisha kiasi kilichofanya waandishi waendelee kuhoji kulikoni juu ya jambo hilo.

Mmoja wa waandishi alisikika akimuuliza Sitti ni kituo kipi alienda kutoa taarifa baada ya cheti chake cha kuzaliwa kupotea ili waende wakafuatilie kujua ukweli na kuwajuza waTanzania.
Hii ni baada ya kuonekana kwa cheti cha kuzaliwa ambacho kimetengenezwa mwaka huu, yani kipyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
Sitti hakuwa na la kujibu na kuzidi kusema waandishi na watu wameendelea kumfuatilia sana maisha yake na hivyo maswali yote waulizwe watu wa Miss Tanzania.

Pia Sitti amekana kutokuwa na mtoto wala stashahada ya uzamiri (Master's Degree) kama ilivyoenea katika baadhi ya mitandao ya kijamii.

Suala la Kumvua Taji
Kamati, ikiongozwa na mwenyekiti HashimLundenga imesema haina sheria wala mamlaka ya kumvua Sitti taji hilo endapo atagundulika amefanya udanganyifu, na kuongeza kuwa ni Baraza la Sanaa (BASATA) na Wizara husika pekee ndo wenye uwezo wa kumvua Sitti taji.

Hadi kikao hicho kinaisha, sio Sitti, wala Kamati ya Miss Tanzania wala mama yake waliokuwa tayari kuzungumzia suala la Passport wala leseni na kuwafanya waandihi wabaki na majibu ya kutoridhisha.

0 comments: