Mheshimiwa Samweli Sitta Akanusha Maneno ya Mh. Joseph Mbilinyi "Mr II Sugu"
Aliyekuwa spika wa Bunge la kutafuta Katiba Mpya, ndugu Samwel John Sitta amekana kutomtafuta mheshimiwa mwenzie Mr II maarufu kama Sugu au lile maalumu la Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya Mjini kupitia CHADEMA.
Amejibu hayo baada ya Sugu kudai kuwa alimtafuta yeye ili ashawishi vijana wa upinzani wampigie kura, hivyo angepitisha mambo mengine pamoja na serikali tatu walizotaka wapinzani akiwa Mwenyekiti.
“Sugu ni mtu gani kwangu mimi hata nimtafute? Nikitaka kuongea na CHADEMA nitamtafuta (Freeman) Mbowe au (John) Mnyika na si Sugu, hata sijui tulikutana wapi na yeye hadi akadai mimi niliomba anipigie kura ili niwe Mwenyekiti wa Bunge la Katiba,” alisema Sitta.
0 comments: