Mtangazaji Ben Kiko wa TBC Afariki Dunia

Mwanahabari mkongwe wa shirika la habari la TBC amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam, Upanga.

Kiko amewahi kuwa mtangazaji wa vipindi mbalimbali enzi za Redio Tanzania na pia ndo mwanahabari wa kwanza kutangaza habari za Vita vya Kagera mwaka 1979.

Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Peponi

0 comments: