Umri Watatanisha Taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu
Sakata kubwa linazidi kuendelea katika mitandao ya kijamii kuhusu taji la Redds Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu na suala la linaloumiza watu vichwa juu ya umri wake.
Habari zimeendelea kutapakaa huku baadhi ya watu wakitoa vielelezo tofauti kuhusu umri wa Sitti na suala lake la kushiriki na kupata taji la Miss Tanzania 2014. Vielelezo hivyo ni pamoja na Pasi ya Kusafiria (Passport), Leseni ya Udereva (Driving Licence) na baadhi ya nakala tofauti zikionyesha kuwa Sitti alizidi miaka 22 ambacho ndo kikomo cha kushiriki miss Tanzania, ukiachilia miaka 18 ya kuanzia.
Taarifa hizo zinazoendelea kwa kasi Instagram, Whatsapp, Facebook na baadhi ya Blog zinazidi kuleta utata kufanya kuwaumiza kichwa waandaaji na wadhamini wa Miss Tanzania, mwenyekiti Hashim Lundenga na timu yake.
Hivi hapa baadhi ya vigezo vinavyoelezwa kuwa Sitti hana miaka 18 bali 25.
Leseni ya Udereva ya Texas, Marekani
Pasi ya Kusafiria (Passport) ya Tanzania
Na Vielelezo Vingine
0 comments: