Kifo cha Sherry Mwana Chazua Utata kwa Mainda

Kifo cha aliyekuwa msanii Sherry Magali a.k.a Sherry Mwana wa bongo movie ambae alitamba katika filamu ya "IN'YE" kimezua utata katika familia yake na kupelekea kuamuathiri kabisa Mainda.

Msanii huyo aliyefariki dunia hivi karibuni mjini Morogoro, anadaiwa kuwa alikuwa akilitaja jina la Ruth Suka 'Mainda' kila mara hadi alipofikwa na mauti.




Inasemekana msanii Sherry alianza kugoma kula akidai hadi amuone msanii mwenzake huyo ambae alikuwa jijini Dar es Salaam anakoishi.

Chanzo kinasema kwamba hata siku aliyofariki pia alilitaja jina hilo, kitendo kilichowaumiza sana baadhi ya ndugu na marafiki. 
Mainda ambae alikuwa ni rafiki wa marehemu, alikiri kusikia jambo hilo na anasikitika kwamba siku aliyopanga kwenda, ndio siku ambayo kipenzi chake huyo aliaga dunia.

Chanzo: Gazeti la Risasi, 5 - 7 Nov, 2014 Uk. 3

0 comments: