Shilole: Haina Shida Nuh Akinipa Mtoto
Msanii wa bongofleva ambae anatamba na video yake mpya ya wimbo "Namchukua", Zena Mohamed a.k.a Shilole ama Shishi Baby a.k.a Mamaa Nuh Mziwanda, amedai kuwa anaweza kufunga kwa kushika ujauzito kwani anatamani kuongeza mtoto wa pili.
Shilole ambae amebahatika kuwa na mtoto mmoja, alisema kuwa pamoja na yote anaamini mtoto aliye nae sasa ni mkubwa hivyo hata akiamua kutafuta mwingine haitakuwa shida kwani anatamani kuongeza familia.
Shilole ambae kwa sasa yupo katika mahaba mazito na msanii mwenzake wa bongofleva anayetamba na wimbo wa "Msondo Ngoma", Nuh Mziwanda, na ndie ambae anatamani ampatie mtoto huyo wa pili.
Chanzo: Gazeti, Lete Mambo 30.14.2014 Ukurasa 2
0 comments: