MEDA Aliyefanya "Barua Kwa Diamond" Aliiba Melody Huku

Yule jamaa anayetokea Iringa anayetamba na wimbo "Barua Kwa Diamond" anayejulikana kwa jina la "MEDA" ambae kwa sasa video yake imekuwa gumzo katika televisheni na mitandao ya kijamii kumbe alichukua melody katika wimbo alioshirikishwa Diamond Platnumz.

Wimbo huo unaoitwa "Ukisinzia" ambao ni remix, wa jamaa wa kuitwa Ken da Swagger na M25 ambao pia walimshirikisha Queen Darleen, una baadhi ya maneno na melody zilizochukuliwa na Meda katika kunogesha wimbo wake wa "Barua"






Baadhi ya maneno "Hello, Hello Darling...." yaliyoimbwa na Diamond katika wimbo wa "Ukisinzia" yamechukuliwa na kubadilishwa kidogo na Meda katika wimbo wake wa "Barua kwa Diamond" kwa kuandikwa "Hello, Hello Diamond....". Yapo hayo na mengine pia.

MEDA









Hebu sikiliza ngoma zote mbili hapa ndo utaelewa kilichofanyika.



0 comments: