Fahamu Jinsi ya Kupiga KURA Tuzo za NYAMBAGO Kanda ya Kati
Tuzo za muziki, utangazaji na filamu za kanda ya kati zilizopewa jina la NYAMBAGO, yani Nyambago Central Awards bado zinaendelea na washiriki wameendelea kuomba mashabiki wao kuwapigia kura kadri wawezavyo ili kuweza kujishindia tuzo hizo ambazo kilele chake itakuwa tarehe 12 Desemba, 2014.
Upigaji wa kura ulianza kuruhusiwa juzi usiku saa 6 tarehe 21.11.2014, na kura zote zitapigwa kwa njia ya sms (ujumbe) kupitia namba ya Zantel, 0773448686.
Baadhi ya Vifupisho vya Maneno ya TUZO katika Upigaji Kura
HP - Hiphop (Msanii bora wa hiphop Kanda ya Kati)
KP - Kizazi Kipya (Msanii bora wa mziki wa kizazi kipya, yani bongofleva)
WB - Wimbo Bora (Hiphop na/au Kizazi Kipya)
MV - Movie (Msanii Bora wa Filamu)
RP - Radio Presenter (Mtangazaji Bora wa Redio, vipindi vya burudani)
na vingine tofauti.............
TUZO ZILIZOPO
1. Utangazaji
Mtangazaji, hasa wa vipindi vya burudani.
Ni watu 4 ndio wamejitokeza kushiriki, wawili wametokea Nyemo Fm Radio 97.7 Dodoma (Winston Makangale na Kasenya) na wawili wametokea Impact Fm 94.4 Dodoma (Willz Snady na mwanadada D Ze Queen).
Jinsi ya Kupiga Kura
Andika NYAMBAGO - RP - Jina la Mtangazaji halafu tuma ujumbe kwenda 0773448686
Mfano:
NYAMBAGO - RP - WINSTON MAKANGALE
NYAMBAGO - RP - WILLZ SNADY
NYAMBAGO - RP - D ZE QUEEN, n.k
Baadhi ya Picha za Watangazaji
2. Msanii Bora na/au Wimbo Bora
Hii imechukua wasanii wa kizazi kipya (waimbaji/bongofleva) na hiphop na baadhi ya wasanii walioingia ni One Six, Brezy, Jaco Beatz, Big Born 90, Kamikaze Cyrill, Jimmy Yeyoo, Bush Man, Mchungaji Zayumba na wengine.
Jinsi ya Kupiga Kura
Andika NYAMBAGO - HP - Jina la Msanii
NYAMBAGO - KP - Jina la Msanii
NYAMBAGO - WB - Jina la Wimbo
Mfano:
NYAMBAGO - HP - MCHUNGAJI ZAYUMBA
NYAMBAGO - HP - JIMMY YEYOO
NYAMBAGO - KP - ONE SIX
NYAMBAGO - KP - KAMIKAZE
NYAMBAGO - KP - JACO BEATZ
NYAMBAGO - KP - BREZY
NYAMBAGO - WB - MY VALENTINE
NYAMBAGO - WB - MAMA LAO
NYAMBAGO - WB - ALOA
NYAMBAGO - WB - AMBULANCE n.k
Baadhi ya Picha za Wasanii
3. Tuzo za Filamu (Movie)
Hii inajumuisha msanii wa filamu na filamu bora
Andika NYAMBAGO - MV - Jina la Msanii au Filamu
Mfano:
NYAMBAGO - MV - MICHAEL NASSORO
NYAMBAGO - MV - ZAITUNI HASSAN
NYAMBAGO - MV - JACQUILLINE MATERU
Baadhi ya Picha za Wacheza Filamu/Movie
PIGA KURA LEO UWAPE SAPOTI NA KUWATIA MOYO WASANII WA NYUMBANI
0 comments: