Video ya "Ndo Yeye" ya Jaco Beatz Iko Mbioni Kutoka, chini ya Erick Backamaza II

Aliyewahi kuwa supernyota Dodoma, 2013, Jaco Beatz a.k.a baba Patra ama Mr Malovedavi, anatarajia kuachia video mpya ya wimbo wake "NDO YEYE" siku si nyingi ndani ya wiki hii.
Video ya wimbo huo imeongozwa na Erick Backamaza kutoka Dodoma ambae pia amewahi kufanya video ya Rotten Blood "Hapakaliki" na One Six "Maya"



Bongo Focus jana iliongea na Jaco Beatz na kusema kuwa maandalizi yashafanyika sasa ni muda wa kuachia video na kuanza fitna na promo katika Tv mbalimbali za Tanzania na nje na kuchafua katika mitandao yote ya kijamii ikiwemo Instagram, Whatsapp, Twitter, Facebook na YouTube.

Jaco Beatz (Msanii a.k.a Mr Ndo Yeye)




















Erick Backamaza (Muongozaji/Video Director)




















Audio ya wimbo huo imefanywa na Elly Da Bway pale Hometown Records.
Je, ushawahi kuisikia?
Hii hapa

0 comments: