NYAMBAGO Awards, Central Zone, 2014 On Fire

Zile tuzo zilizokuwa zinasubiriwa kwa hamu kwa wasanii (nyimbo na filamu) na watangazaji zinazidi kupamba moto kanda ya Kati.

Tuzo hizo zinashorikisha mikoa ya kanda ya kati ikiwemo Dodoma, Singida, Morogoro na Iringa ndo zimeanza rasmi hivyo siku si nyingi zile namba (code) za kupigia kura zitatolewa kumchagua msanii umtakae.



Baadhi ya wasanii waliongia ni Cyril Kamikaze "Aloa", Jaco Beatz "Ushindwe Wewe", One Six "Wajua", Mchungaji Zayumba "Aliniacha Mwaka Jana", Brezy "Mama Lao", Jimmy Yeyoo "Hamjanijua", Winston Makangale wa Nyemo Fm Radio "Utangazaji", Willz Snady na D Ze Queen wa Impact Fm "Utangazaji" na wengine kibaaaaaaao wa fani mbalimbali kama vile filamu.

Watayarishaji wa mziki (music producers) hakuna aliyeshiriki hata mmoja hivyo tuzo hizo kukosa watu kabisa, na kundi la Dom Down Click (DDC) pia wamegoma kabisa kushiriki.

Baadhi ya wasanii kama vile Raph Tz na wengine walichelewa kurudisha form hivyo kukosa nafasi ya kushiriki.

Kilele cha Tuzo hizo ni tarehe 12 Desemba 2014.

0 comments: