Rachel Njingo: Msanii Mpya Ajae Bongo Movie

KinKwin Creative Production wanamtambulisha mrembo mwingine mwenye kipaji kwenye tasnia ya Bongo movie ajulikanae kwa jina la Rachel Njingo. Ambaye utapata kumuona katika filamu yao mpya "CLARITHA" ambayo ndani ya filamu hiyo amecheza pamoja na Mohammed Fungafunga a.k.a Jengua , Stanley Msungu na wengineo. 

Filamu hiyo inazungumzia mambo mengi ambayo utapata kuyajua pindi uionapo. Akiongea na Mwinyi Blog, Rachel Njingo amesema filamu hiyo inatarajiwa kuingia sokoni kuanzia weekend ya wiki ijayo. Hivyo wapenzi wote wa filamu wakae mkao wa kula maana chakula kitamu chenye viungo mbalimbali kimeishaiva.














0 comments: