Ujio wa Ngoma Mpya ya Baby Boy "Nisamehe"

Edson Wilson a.k.a Baby Boy ni mmoja kati ya wasanii wakali wa miondoko ya kufokafoka ambae aliwahi kupata umaarufu baada ya kufanya ngoma ya "One Love" aliyoshirikishwa na Steve RnB.

Baada ya kukaa kimya muda mrefu, Baby Boy ameamua kuvunja ukimya kwa kufanya ngoma mpya inayokwenda kwa jina la "Nisamehe" akiwa na Wynem.




Mdundo/beat ya ngoma hiyo imefanywa na Nuh Mziwanda a.k.a Baba Shishi na baadae mixing kufanywa na Jaysson ndani ya studio ya Kali Nation iliyopo Makumbusho, Kijitonyama, Dar.

Inasemekana Baby Boy amepanga kufanya video chini ya kampuni ya video ya After DayLight Films chini ya muongozaji Raph Tz mwishoni mwa mwezi Januari ambayo itaambatana na audio ya wimbo wake huo.

Sikiliza kipande/intro ya wimbo huo "Nisamehe" huku akiwataka mashabiki wake kukaa tayari


0 comments: