Video ya Nasema Nawe ya Diamond Platnumz Yapigwa Marufuku

Video ya wimbo wa msanii mkali wa bongofleva, yule Rais wa Wasafi wa kuitwa Chibu Dangote the Platnumz, Diamond ama Baba Zari akiwa na malkia wa mipasho Khadija Kopa imepigwa marufuku kunoneshwa ktk televisheni mbalimbali za nchini Tanzania.

Video ya wimbo huo "Nasema Nawe" iliyoongozwa na Hanscana inasemekana imepigwa marufuku baada ya kukiuka maadili ya kiTanzania kwa kuwemo wadada wanaocheza kwa kutingisha makalio yao kihasarahasara.



Hebu angalia video hiyo ujionee mwenyewe balaa lake.
Ni video kali, iliyotayarishwa vizuri ila tatizo ndo hao wadada ambao wapo mwishoni mwa video hiyo.



0 comments: