Raph Tz Akiimba "Wa Moro" ya Jordan

Kati ya mambo ambayo huwashangaza watu ni msanii na muongoza video wa nyimbo za bonngofleva, Raph Tz kuonekana kupenda nyimbo za wasanii wenzake na hata kufikia kuziiga na kufanya video clips akionekana kuziimba au kuzifanya kiustadi.

Ukiacha wimbo wa Bongo Dar es Salaam wa Prof J akimshirikisha Lady J Dee aambao aliachia clip yake siku kadhaa nyuma akirap verse ya mheshimiwa mtarajiwa, Raph Tz sasa ameamua kuachia clip ya wimbo wa msanii Jordan a.k.a Majo a.k.a Kanyongakitu unaoitwa "Wa Moro".

Wa Moro ilifanyika Rockatiz Records kwa Tris, miaka kadhaa nyuma, ikiwa ni moja kati ya ngoma kali sana zilizowahi kufanywa na Jordan Kanyongakitu, ukiacha na "Wasiwasi" aliyofanya na Belle 9 na Ben Pol, "Nanenepa" aliyofanya na Lotty, "Mapenzi Ni Vita" na nyingine nyingiii kali.



Jordan a.k.a Mr Kanyongakitu
Alivyoulizwa Raph Tz kwa nini ameamua kufanya clip hiyo, akasema hivi; 
"Unajua Jordan ni mshikaji wangu sana, ni jamaa ambae nimekuwa nae na kuishi nae kitaa kimoja na harakati zake za mziki na uwezo wake nauelewa. Wa Moro ni moja kati ya ngoma zake nazozielewa sana, na nikaimiss tu kusikiliza nikaona si vibaya nikafanya clip ya verse ya kwanza na kiitikio'

Kwa nini na sio wasanii wengine?
Raph Tz akasema; "Napoona ngoma naipenda, napenda kuonyesha jinsi gani naikubali na kupitia clip za kujirekodi, basi naiimba au narap kushow kuikubali"


Hebu angalia Raph Tz alivyofanya ngoma ya Jordan Kanyongakitu


0 comments: