Professa Mbarawa Azindua Nembo Mpya ya TTCL

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi,mheshimiwa mbunge Professa Makame Mnyaa Mbarawa amezindua nembo mpya ambayo itatumika na kampuni ya simu Tanzania,TTCL.

Akiwa mbele ya viongozi wa TTCL, wafanyakazi pamoja na waandishi wa habari alipokaribishwa katika sherehe za uzinduzi wa huduma ya 4G na nembo mpya ambao ulifanyika mbele ya ofisi za TTCL zilizopo mtaa wa Samora, Dar es Salaam, amehasa watumishi wa TTCL kujikita katika uwajibikaji na mabadiliko kutokana na kubadilika kwa nembo ya kampuni yao ambayo imekuwa kampuni mama ya simu tangu mwaka 1994 na miaka ya nyuma. Amewataka vijana kujituma zaidi na kutaka watumishi wa zaidi ya miaka 40 kuwaachia vijana nafasi waweze kuisukuma TTCL mbele ili kuleta ushindani na kampuni nyingine za simu.

"Naona vijana ni wengi na ushindani wa sasa unahitaji hasa vijana ili kuleta ushindani. Najua kesho mtanijadili sana lakini ukweli utabaki pale pale, vijana chini ya miaka 40 ndio watakaoikomboa TTCL.

Nembo mpya ya TTCL






















Nembo ya zamani ya TTCL




0 comments: