Video | Goodluck Gozbert - Nibadilishe

Baada ya kuamua kuachana na utunzi na utayarishaji wa muziki wa bongofleva na kujikita zaidi katika uandishi na uimbaji wa nyimbo za Injili, msanii Goodluck Gozbert, ambae zamani alifahamika kama Lollipop, hivi karibuni ameachia video ya wimbo wake wa "Nibadilishe".

Ni moja kati ya nyimbo kali za dini uliochanganya ladha za mziki wa kizazi kipya na staili fulani kutoka nchi jirani ya Kenya.

Si ufundi tu, hata kipaji na baraka za Mungu zimeendelea kummiminikia kijana huyu anayeaminika kuwa ni mmoja wa vijana wanaofanya vizuri sana ktk kazi ya sanaa ya mziki wa Injili.
Hii hapa video ya Nibadilishe.

0 comments: