Ali Kiba, Baba Levo, Blue Bayser, Dully na Mchungaji Zayumba Wafunika Fiesta Dodoma, 2014

Ile show ya kuzunguka zaidi ya miji 18 Tanzania iliyokuwa na inayoendelea kusubiriwa na mashabiki wengi mikoani, FIESTA, inayodhaminiwa na bia ya Serengeti chini ya kampuni ya bia ya Serengeti na Clouds Media Group hatimae ilikita Dodoma siku ya Jumapili ya Oktoba 5, 2014.
Mashabiki wengi walijitokeza kushuhudia wasanii wao wakifanya vizuri na kuonekana kushangilia sana baadhi ya wasanii kadhaa kwa kufanya vizuri.
Bongo Focus na timu nzima ilikuwepo na kuona msanii Mchungaji Zayumba anayewakilisha Dodoma akichuana vikali na wakali ambao walishakuwa na majina katika upande wa ushangiliwaji.
Zayumba alipata usawa wa shangwe sawa na Dully Sykes, Mr Blue Babylon Byser, Baba Levo na Ali Kiba ambae watu walimsubiri kwa hamu kubwa akifanya wimbo wake wa "Mwana Dar es Salaam" unaozidi kutesa redio mbalimbali za Tanzania.
Wengine waliofuatia kupata shangwe ni Mo Music, Young Killer na Fid Q.
Dully Sykes
Blue Babylon Byser
Ali Kiba
Young Killer
Mo Music
Jux
Shangwe za Fiesta 2014 kilele chake ni tarehe 18 Oktoba 2014 zitakazofanyika pale Leaders Club, na msanii T.I kutoka Marekani atakuwepo

0 comments: