Hatimae Rasimu ya Katiba Yakabidhiwa Leo kwa Rais, Dodoma
Baada ya mchakato mzima wa kumalizika kutunga katiba inayopendekezwa na Bunge la Katiba 2014, hatimae shughuli za kukabidhi katiba hiyo zitafanyika leo mjini Dodoma katika Uwanja wa Jamhuri.
Baada ya kazi ngumu na kubwa iliyofanywa na Tume ya Jaji Warioba kwa kutafuta maoni, halafu Bunge la Katiba kushughulikia upendekezaji na urekebishaji wa vipengele, sasa ni kazi ya Wananchi ndo imebaki kupitisha katiba hiyo kwa maoni. Akishakabidhiwa mheshimiwa Rais Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, ndipo itapelekwa na wananchi.
0 comments: