Jaco Beatz na Raph Tz ndani ya Bongo Page ya Dj Rodger, ABM Radio 91.2 Dodoma

Ilibahatika ndani ya siku moja wasanii wakali wawili kutokea Dodoma, yani Jaco Beatz na Raph Tz wakihojiwa kwa pamoja katika kituo cha redio cha mjini Dodoma, ABM Fm 91.2 katika kipindi cha Jumamosi cha Dj Rodger, yani Bongo Page.
Jaco Beatz alikwenda kuzungumzia ngoma yake "NDO YEYE" na harakati zingine za mziki, vivyo hivyo kwa Raph Tz alikuwa ananukisha ngoma mbili, "JIPANGE" aliyofanya na Tundaman na Darasa, na "I CAN" alowashirikisha One Six, Uncreakable na Miracle.
Hii hapa.
 

0 comments: