Je Wamfahamu Rapper/Mwana-Hiphop Tajiri Duniani?!
Imekuwa kila siku watu na washabiki wa mziki wa hiphop duniani kupendelea kufuatilia utajiri wa wanamziki hao na jinsi wanavyolinganishwa miaka kwa miaka.
Jarida la Forbes (Forbes Magazine) mnamo tarehe 5 Mei mwaka huu 2014 likaamua kutoa 5 Bora za wana-hiphop matajiri kuliko wengine na kuainisha kiasi cha fedha wanazomiliki na ukuaji wa vipato vyao kadri miaka inavyozidi kwenda.
5 bora hiyo iliitwa "The Forbes Five|" na inaainisha kuwa Sean Com "P Diddy", Dr Dre, Jay Z, Birdman "Baby" na 50 Cent ndo wana-hiphop matajiri kuliko wote duniani.
P Diddy anaongoza kwa kumiliki Dola Million 700 za Kimarekani (Sawa na Shilingi za kiTanzania 1,177,050,000,000 yani Trilion Moja Bilioni Mia Moja na Sabini na Saba na Milioni Hamsini) ambapo Dolla Million 120 zimeongezeka mwaka jana hadi kufikia hapo. Hiyo ni kwa kulingana na badiliko la fedha leo tarehe 8.10.2014, yani Dola 1 = Tsh 1681.5.
Akifuatiwa na Dr Dre na Jay Z wenye utajiri wa Dolla Million 550 kwa 520.
List Below, from left there is P Diddy, Dr Dre, Jay Z, Birdman & 50 Cent
0 comments: