Je, Ngoma ya Jaco Beatz, Brezy Chocolate na Wise One Zafanana?
Imekuwa swali la wasikilizaji na mashabiki wengi wa muziki wa wasanii (fans) wa Jaco Beatz, Wise One na Brezy Kinyangoroka kuhusu kufanana kwa ladha ya ngoma mpya zilizoachiwa na wasanii hao wakali watatu wakitokea Dodoma.
Wengine wamekuwa wakisema labda ni sababu ya ukaribu wa jamaa hao watatu na sababu nyingine ni za kusema eti kwa vile walishawahi kufanya kazi studio moja ya Choice Records ailiyokuwaga Barabara ya 6 Dodoma, pia wapo wanaothibitisha kuwepo kwa maneno yanayofanana katika nyimbo hizo tatu zilizofanywa sehem tofauti.
Je, kweli zafanana?
Ndo Yeye - Jaco Beatz (Prod. Ely da Bway @Hometown Records)
Kidogo - Wise One (Prod. Sailas @Dreamz Records)
Mama Lao - Brezy (Prod. Kimambo Touches @Chapakazi Records)
Hebu sikiliza mwenyewe
0 comments: