Ngoma ya Raph Tz "I CAN" Yavuja

Ngoma mpya wa msanii wa kufokafoka akiwakilisha Dom na Dar, Raph Tz, yavuja. Ngoma hiyo haikuwa hata na siku nyingi tangu ifanywe na Lil Bello Bin Laden pale AJ Records.
Akizungumza katika kituo cha redio cha ABM 91.2 Dodoma, katika kipindi cha Bongo Page cha Jumamosi kinachoendeshwa na Dj Rodger, Raph Tz asema hakuwa amepanga kuachia "I CAN", ila imevuja na tayari ishaanza kuwepo katika library na baadhi ya redio za Dodoma.
Ndani ya ngoma hiyo Raph amewashirikisha One Six, Uncreakable na Miracle.
Raph Tz alipanga kuachia ngoma yake ya "JIPANGE" aliyofanya na Tunda na Darasa, ndipo "I CAN" ifuate baada ya muda. Pia amesema si mbaya ngoma hiyo kuvuja mana imekuwa kama utaratibu wa wasanii kuachia ngoma mbilimbili kipindi hiki kama alivyofanya Prof. Jay, Yamoto Band n.k.
Msikie Raph hapa.


0 comments: