Je Unafaham Nyimbo Zilizompa Umaarufu Juma Nature?!
Wakati wasanii wa siku hizi wakitamani kutoka haraka haraka katika muziki, wakongwe kama Juma Nature a.k.a Sir Nature au Kibra, walikuwa wakigangamara sana hadi kupata umaarufu na kuhakikisha kila siku wamekuwa wakifanya kazi nzuri kuendelea kuwepo hewani.
Juma Nature ambae umaarufu wake ulisaidiwa sana na Dj JD au John Dillinga Matrlou hasa kipindi akiwa anaendesha kipindi cha The Crews cha East Africa Radio.
Ukiachilia nyimbo alizofanyaga zamani, Juma Nature alianza kujizolea umaarufu hasa katika nyimbo alizotengeneza chini ya mtayarishaji P Funk a.k.a Majani a.k.a Kinywele Kimoja katika studio za Bongo Records zilizopo jijini Dar es Salaam, Bamaga kati ya Mwenge na Sinza. Nyimbo hizo ni kama vile Jinsi Kijana, Kighetogheto, Sonia, Sitaki Demu, Inaniuma Sana na nyingine nyingiiiiii.
Jinsi Kijana ndo wimbo uloanza kuonyesha njia kwa Juma Nature ingawa tayari alishaonekana kuwa msanii mzuri hasa baada ya kushirikishwa na wasanii wenzake kadhaa na kufanya vizuri katika viitikio.
Jinsi Kijana, Hili Gemu, Sonia na Kighetogheto zilipewa umaarufu na East Africa wakati Sitaki Demu ilipewa sana umaarufu na Redio Clouds.
Hizi hapa baadhi ya ngoma za Juma Nature enzi hizo
Jinsi Kijana, Hili Gemu, Sonia na Kighetogheto zilipewa umaarufu na East Africa wakati Sitaki Demu ilipewa sana umaarufu na Redio Clouds.
Hizi hapa baadhi ya ngoma za Juma Nature enzi hizo
0 comments: