Ndo Yeye wa Jaco Beatz Kumbe Fundi

Imekuwa kawaida kwa baadhi ya watu wanaopata majina kuweka hadharani juu ya mahusiano waliyonayo lakini kuficha ukweli mambo yanapoharibika.

Hii imekuwa tofauti kwa aliyewahi kuwa SuperNyota wa Dodoma, 2013, msanii Jaco Beatz aliyefunguka kuhusu sakata la mahusiano yake. Japo kwa kupindishapindisha maneno lakini Bongo Focus ilibaini kuwa Jaco Beatz na mpenziwe Cleopatra Paulsen a.k.a Patra wako katika wakati mgumu kimahusiano.

Pia Jaco anazidi kumsifia kuwa mpenziwe ni fundi wa malovedavi na anaamini siku zote amekuwa ndiye hasa chaguo lake.
Jaco ambae anategemea kuachia video yake ya wimbo "Ndo Yeye au Ngebe" chini ya muongozaji Erick Backamaza wa After DayLight Films.



Jaco Beatz enzi za mapenzi motomoto na Patra Paulsen






















0 comments: