Wajua Diamond Platnumz Atakuja na Nani kwa Matei Lounge, Dodoma?!!!!
Mkali wa bongofleva Diamond Platnumz a.k.a Chibu Dangote ama Mr Mdogomdogo anategemea kutua na timu ya watu kibao katika show ya kwa Matei Lounge inayotarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 11.10.2014 kipande cha Area D, Dodoma.
Ukiachilia Onyinye wake binti Sepetu, na WCB Dancers, mkali huyo anategemewa kuja na list ya mabinti kutoka Wasafi Classic kunogesha show hiyo izidi kufana zaidi.
Licha ya kuwepo kwa kiingilio kidogo cha 30,000 - 40,000 bado mashabiki watafurahia show kali na mandhali nzuri ya Matei Lounge.
0 comments: