Dj Man Yuzo na Dj Amiry, maDJ Wakali Dodoma

Kama ushawahi kuja Dodoma na kutembelea viwanja vya kula bata nadhani utakuwa umewahi kusikia maDJ wakali wawili, Dj Man Yuzo na Dj Amiry.

Hawa ni ndugu kabisa na ndo mana wanajiita Blood DJs.







Dj Man Yuzo: 
Anafanya kazi kama DJ pale Nyemo Fm Radio 97.7 Dodoma katika vipindi mbalimbali kikiwemo Full Nyemo Exclusive, kwa pamoja wakikisanua na mtangazaji machachari Winston Makangale.

Pia Dj Man Yuzo a.k.a Yuzo mkali huwa anahusika sana kipande cha Maisha Club Dodoma akiungana na maDJ wengine wenzake wakali kuwapa mzuka wanaokuwa kipande kile.



Mara nyingi amekuwa upande wa VIP kule juu, na chini huwa anashikawakati wa ngoma kali za mwisho mwisho mida ya 9 usiku.
Mwenyewe anajiita "The Entertainer".

Dj Amiry:
Huyu ni mmoja kati ya maDJ matata sana ukienda viwanja.
Kwa sasa Amiry ni Dj pale Matei Lounge & Car Wash pande za Area D, Dodoma na ndo huwa ananukisha show zote za kuanzia saa 1 usiku.

Pia ameshawahi kuwa DJ wa Club Laaziz ya Makole, Dodoma na kuna kipindi anapata shavu la kukinukisha pande za Maisha Club.













0 comments: