Ujio wa Armstrong & Bandago wakiwa na Wynem ndani ya "Mamzekee", J3 Tar 24.11.201

Kama ushawahi kusikia wimbo wa "MICHANO" basi utakumbuka Armstrong na Bandago ni kina nani.

Ni zaidi ya miaka 10, tangu wafanye wimbo wa pamoja "Michano" wakiwa watangazaji wa redio Clouds, Armstrong na Bandago wameamua kurudi tena kuja kuteka soko la mziki wa bongofleva kwa ngoma yao mpya "MAMZEKEE" inayotarajiwa kutoka jumatatu, 24.11.2014 wakiwa na Wynem.



Kwa mashabiki hii itakuwa kama surprise na zawadi kubwa toka kwa jamaa hao wawili tangu wafanye ngoma ya pamoja iliyofanywa vilivyo na marehem Complex akishirikiana na Nice P, mwaka 2004 pale Namanga, Msasani, Dar es Salaam ilipokuwa studio ya Backyard Production.

BANDAGO
Bandao ameshafanya wimbo unaitwa "Achana na Demu Wangu" aliowashirikisha Banana na Maulo.

















Na kama unapenda mziki mzuri, basi huwezi kumtaja Wynem kwa wakali wanaofanya poa katika bongofleva tangu enzi hizo.

Wynem amaeshiriki kufanya viitikio vya nyimbo mbalimbali kama vile "Kauli Safi" na "Hisia Zangu" za Raph Tz, "Nisamehe" ya Baby Boy, "Sms" ya Nick Maujanja na nyingine nyingi. Pia ashawahi kufanya nyimbo kadhaa na Linex zikiwemo "Maumivu" na "Japo Kidogo" na ameshafanya ngoma zake peke yake kama vile "Mwanambuzi" na "Utata"










ARMSTRONG DADDY

















Kwa hiyo kwa muunganiko wa watu watatu, "MAMZEKEE" itakuwa ni habari ya mjini.

Kaa Tayari.....ni JUMATATU, 24.11.2014

0 comments: