Video Interview ya Miracle Akiongelea Mixtape "The Element II" ya DDC iliyofanywa na Duke
Kama unapenda muziki wa hiphop kutoka Dodoma, basi ukiambiwa DDC (Dom Down Click) nadhani hutopata shida kufaham ni vitu gani wanafanya.
Wako mbioni kuachia kanda mseto (MIXTAPE) inayokwenda kwa jina la "The Element II" mnamo tarehe 29.11.2014 ambayo imefanywa na DUKE.
Taarifa hizo zimetolewa na mmoja wa kundi hilo, Miracle, katika interview aliyofanyiwa akiwa katika studio za AJ Records, Area C, Dodoma.
DDC inajumuisha wasanii kama vile Andre K, Adam Shule Kongwe, Goda, Gilson, Slogan, Miracle, Javan, Saliloo a.k.a Saliflow na wengine
Kazi za mixtape hiyo zimefanywa studio mbili, AJ Records na M-Lab, yani DDC na TAMADUNI Music huku zikisimamiwa kwa ufasaha na DUKE Touches.
Muone Miracle hapa chini akiongelea mixtape hiyo.....
0 comments: