Uzinduzi wa Mixtape "The Element Vol II" ya DDC, 28.12.2014

Kama uko Dodoma na pande zote za karibu na maeneo hayo ya mjini, tarehe 28.12.2014 siku ya Jumapili kutakuwa na uzinduzi wa mixtape 'kanda mseto" ya wanahiphop DDC (Dom Down Click) kutoka Dodoma.

Uzinduzi utafanyika ndani ya ukumbi wa N.K karibu kabisa na kituo cha daladala cha Jamatini, kuanzia saa 8 Mchana hadi saa 3 Usiku.

Mlango unalipia Buku 3 Tu.

Nash Mc, Duke, Central Zone, Mazichi, One Six, Rap Nation na Ostezee Ving'ang'a watakuwepo.

0 comments: