Fahamu Kazi za Muongoza Video (Video Director) Nisher

Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. 

Nisher amekulia katika maisha mazuri na hadi sasa ni wakishua bado. 

Baba yake aliweza kumsaidia Nisher kufungua studio yenye thamani kama ya milioni 15 ili mtoto wake aendeleze kipaji alichonacho.


Nisher amefanya video nyingi sana za mziki wa bongofleva na inasemekana ndo muongozaji wa video anayetoza pesa nyingi zaidi katika kufanya kazi zake na ni kweli kila kazi ya Nisher unayoiona, unaona kabisa utofauti na kazi alizowahi kufanya kipindi anaanza.

Amekuwa ni muongozaji mkubwa wa video za Weusi (Joh Makini, Nikki II & G Nako), na kama ujuavyo watu wa Arusha wanapenda kubebana sana.

Wasanii wengine aliowahi kuwafanyia video ni hawa...

  • BenPol - Unanichora & Jikubali
  • Fid Q - Bongo Hiphop
  • Nasry - Nini
  • Baraka da Prince - Jichunge
  • Young Killer ft. Fid Q - 13
  • Feza Kessy - Amani ya Moyo
  • Na nyingine nyingi

0 comments: