Kampuni ya Mabasi ya Shabiby Yaleta Mabasi Mapya ya Kisasa, Dar - Dom - Dar

Kampuni ya mabasi yaendayo mikoani hasa Dodoma yakitokea Dar imeleta mabasi mapya na ya kisasa kabisa ambayo inasemekana yataleta ongezeko la wateja wengi sana kwa muonekano wake huo mpya.

Mabasi hayo ambayo nauli yake inategemea kuwa na tozo la shilingi 35,000 za kiTanzania kwa safari ya Dar es Salaam kwenda Dodoma au Dodoma kwenda Dar es Salaam.


Mabasi hayo yenye Tv na vifaa vya kusikilizia (headphones) katika kila kiti (seat) bila kusahau AC (Air Condition) yatakuwa kivutio kikubwa kwa wapandaji hasa kupunguza uchovu wa safari na kumfanya mteja afurahie safari yake. 

Pia yana choo ndani cha kuwezesha watu kujisaidia wakati gari linaondoka bila kusimama na kufanya safari isiwe ya kusimama simama.

Gari hizo pia zimefungwa "WIFI" inatakayosaidia upatikanaji wa internet njia nzima kwa wateja wenye sim za smartphone/android kuendelea kufurahia huduma wakiwa ndani ya basi.

Inasemekana gari hizo zitaanza rasmi safari zake kuanzia Jumatano ya tarehe 22 July 2015.

Angalia picha za ndani za mabasi hayo


















0 comments: