Mfahamu Msanii wa Bongofleva "Mchaji Halisi"

MAISHA YAKE
Herry Wilbard ama "Mchaji" ama "Mchaji Halisi" ni mmoja wa wasanii wa bongofleva wenye uwezo mkubwa kimziki lakini waliokosa bahati ya kusikika katika gemu ya mziki nchini Tanzania.

Mchaji, ambae zamani alikuwa akitumia jina la Rwid B ikiwa ni kuunganisha na kufupisha herufi za jina lake ili kuleta ladha katika utamshi, amezaliwa February, 3.



Kwa sasa Mchaji anaishi maeneo ya Kigogo Mbuyuni, lakini zamani alikuwa anaishi maeneo ya Mabibo, ambako kuna chimbuko la wasanii wengi wakiwemo Pingu na Deso, Suma Mnazalet, Solid Ground Family, JobisoMalee na wengine wengi.

HARAKATI ZA MZIKI
Mchaji ni mmoja kati ya wasanii wachanga ambae aliwahi kufanya kazi studio tofauti ndogo na kubwa na ma-producer wengi wadogo kama vile Jaysson na wakubwa kama vile Bizzman, Enrico, Maco ChaliMika Mwamba, Said Comorien na wengine wengi, pia ashafanya kazi na mastar tofauti wakiwemo Madee na wengine, katika harakati za kukuza kipaji chake.

Mchaji alishawahi kuwa katika kundi la WASONATA lililounda wasanii wanne yani Lotty, Mchaji, Raph Tz na Ibro na wakafanikiwa kufanya ngoma iliyoitwa "Mrembo" katika studio ya Fabrice Records iliyokuwa Mwananyamala, Dsm, ingawa katika ngoma hii Lotty hakuwemo. Pia baadae alijiunga na kundi lingine lililoitwa Wachaji Zote na ndo huko alipopata jina la Mchaji Halisi baada ya kufanya wimbo "Nibembeleze" kwa Said Comorien.

Kwa sasa, ukiachana na harakati za uimbaji, Mchaji anajihusisha na utengenezaji/utayarishaji wa mziki (music producer) na hata baadhi ya nyimbo zake anazofanya sasa amezifanya mwenyewe katika studio tofauti tofauti.

Hebu sikiliza, download na share baadhi ya nyimbo za Mchaji hapa chini....


0 comments: