New Audio: Roma ft. One Six, Chibwa & Walter Chilambo - Viva Roma

Mwanaharakati na mwanahiphop kutoka Tanzania, Roma Mkatoliki ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la "Viva Roma".


Ndani ya wimbo huo ameshirikishwa mkali wa RnB na Sweet Reggae ambae pia ni mdogo wa marehemu Mez B anayekwenda kwa jina la One Six.


Pia wamo Chibwa yule mkali wa Ragga Dancehall na bila kumsahau aliyewahi kuwa mshindi wa Bongo Star Search, Walter Chilambo.

Wimbo huo ambao umesheheni habari nyingi za siasa, viongozi na harakati kama hizo na ni maalum hasa kwa kipindi hiki kuelekea Uchaguzi.

Baadhi ya redio zimegoma kupiga wimbo huo, lakini Roma mwenyewe haogopi na amesema atausambaza hadi ufikie walengwa.

Kutoka Tongwe Records, hii hapa Viva Roma ya Mkatoliki.


0 comments: