New Video: Man Chipi ft. Benah - Sio Kama Wale

Man Chipi ama anavyopenda kujiita mwenyewe "Wa Ming'azo" ni mmoja kati ya wasanii wanaochipukia anayewakilisha mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara.

"Sio Kama Wale" ni ngoma yake mpya na amefanyiwa video na muongozaji Lax Lilah, wakati video hiyo ikiwa imehaririwa na Raph Tz wa RTZ Media Lab.



Audio ya ngoma hiyo imefanyika pale Kali Nation studio chini ya mtayarishaji Chriss FrayKay ambae pia alifanya ngoma ya "Mfalme wa Subira" ya Raph Tz.

Ndani ya "Sio Kama Wale" ameshirikishwa Benah, msanii mkali anayechipukia na mkali wa viitikio na ukali wake unadhihirika katika wimbo wake wa "Mbali Nami".

Hii hapa video ya Sio Kama Wale ya Man Chipi.


0 comments: